Skip to main content
Skip to main content

Polisi Malindi wafungua uchunguzi baada ya miili ya wanaume wawili kupatikana kando ya barabara

  • | Citizen TV
    1,391 views
    Duration: 2:14
    Polisi mjini Malindi wameanzisha uchunguzi kutanzua vifo vya wanaume wawili ambao miili yao ilipatikana imetupwa kando ya barabara kuu ya Mombasa kuelekea Malindi Jumamosi asubuhi. Wakazi wanasema miili hiyo miwili iligunduliwa kwenye kichaka umbali wa mita chache kutoka barabarani. Shirika la Vocal Africa limeelezea wasiwasi kuhusu ongezeko la hivi karibuni la vifo vya kutatanisha katika eneo hilo na kutoa wito wa uchunguzi wa haraka.