Polisi wameonywa dhidi ya kuchukua hongo

  • | Citizen TV
    711 views

    Tume ya huduma kwa maafisa wa polisi Imewaonya maafisa wa usalama dhidi ya kuchukua hongo wakati wa zoezi la kusajili makurutu wa polisi linalotarajiwa nchini. Mwenyekiti wa tume hii Eliud Kinuthia akionya kuwa hatua kali zitachukuliwa kwa watakaokosa nidhamu. Aidha tume hiyo imeeleza kwamba imeweka mikakati ya kutosha ili kukabiliana na visa vyovyote vile vya ufisadi vitakavyoshuhudiwa wakati wa zoezi hilo.