Skip to main content
Skip to main content

Polisi wametawanya waandamanaji Kimara

  • | BBC Swahili
    37,785 views
    Duration: 29s
    Polisi jijini Dar es Salaam wametawanya kundi la vijana waliokuwa wakijaribu kuandamana katika eneo la Kimara Kibo, umbali wa kati ya Ubungo na Kimara, wakati huu wa uchaguzi mkuu unaoendelea nchini. Mashuhuda wamesema kundi hilo la vijana lilianza kujikusanya karibu na Kanisa la Ufufuo na Uzima, ambalo lilifungiwa hivi karibuni. Kanisa hilo la Askofu Josephat Gwajima, ambaye alikuwa mbunge wa chama tawala, CCM, kuanzia mwaka 2015 hadi mwaka huu.- - - #bbcswahili #kura #siasa #maandamano Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw