- 3,728 viewsDuration: 22sNani kama mama? Mtazame mama pomboo mwenye huzuni akibeba mwili wa mtoto wake aliyekufa kwa siku kadhaa, katika kipindi cha maombolezo. Pomboo huyo aitwaye Fraggle amepoteza watoto wake wanne wa mwisho. Video iliyorekodiwa na shirika la Australia, Geographe Marine Research, kwa kutumia droni inaonyesha kundi la pomboo wenzake likimzunguka na kumuunga mkono katika kipindi hicho kigumu. Pomboo wanaweza kubeba watoto wao waliokufa kwa muda wa siku kadhaa kama sehemu ya mchakato wa maombolezo na hulazimika kuwaacha na kuendelea kutafuta chakula ili waweze kuishi. #bbcswahili #Pomboo #Baharini Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw