Raia 10 wa kigeni na mkenya mmoja wametambuliwa kuwa waathiriwa wa ile ajali ya ndege iliyotokea leo asubuhi katika kaunti ya Kwale. Kati ya waathiriwa hao kumi na moja, wanane ni raia wa Hungary, wawili raia wa Ujerumani pamoja na mkenya mmoja. Kwenye taarifa, kampuni ya Mombasa Air Safari ilisema moja ya ndege zake yenye nambari za usajili 5Y-CCA, ilikuwa katika safari yake ya kawaida kutoka uwanja mdogo wa ndege wa Diani kuelekea Kichwa Tembo katika mbuga ya kitaifa ya Maasai Mara ilipoanguka.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive