Raia wa Palestina waelezea hali ngumu ya maisha huku Israel ikiendelea na mashambulizi

  • | VOA Swahili
    331 views
    Raia wa Palestina waliokimbia makazi yao na kuishi kwenye hema eneo la Khan Younis Gaza wameelezea hali ngumu ya maisha huku Israel ikiendelea kushambulia maeneo yanayotawaliwa na Hamas kwa mashambulizi ya anga. Watu wanaishi ndani ya kambi hiyo walisema walikaa kwenye mahema ambayo yamejaa maji mvua inapowanyeshea huku wakisubiri kwa muda mrefu kutumia vyoo na wanapata chakula na maji kidogo. "Natamani Mungu atuonee huruma na vita visimame," Rami Al-Erqan, ambaye anaishi kwenye hema na mke wake na watoto sita, alisema. "Tulifikia hali ambayo tulitamani tungekufa chini ya vifusi ili tupumzike. Maisha yetu ni ya dhiki,” aliongeza. Wanajeshi wa Israel siku ya Jumamosi (Oktoba 28) walitoa wito kwa Wapalestina kuondoka kaskazini mwa Ukanda wa Gaza kabla ya operesheni inayokaribia ya Israel. Israel inadai kuwa Hamas imeweka silaha na vikosi vyake miongoni mwa raia, na imekuwa ikiwaambia wakaazi wa Gaza kuhamia kusini kwa usalama wao. Zaidi ya watu milioni 1.4 wa Gaza wamekimbia makazi yao na kukaa kwenye makazi ya muda kufuatia mashambulizi makubwa sana ya mabomu yaliyowahi kufanywa na Israel. #israel #palestine #gaza #reels #igreels #videography #voa# #hamas #idf