Raia wa Sudan wamekwama katika mji wa Omdurman kutokana na vita vinavyoendelea nchini humo

  • | VOA Swahili
    247 views
    Raia wa Sudan wamekwama katika mji wa Omdurman katika vita vinavyoendelea kati ya kikosi cha Rapid Support Forces – RSF na jeshi la Sudan wamekuwa wakijitahidi kupata fursa ya huduma za matibabu wakati huduma za afya zinaendelea kuvunjika. Khadija Riyami anaisoma ripoti zaidi. Huku kukiwa na uhaba mkubwa wa dawa muhimu, hasa kwa watu wenye magonjwa sugu, baadhi ya wagonjwa wameathiriwa na matatizo kama vile kukatwa viungo, mkuu wa kituo cha afya cha Al Thawra amesema. Ukosefu wa vifaa vya matibabu vya kutosha ikiwemo sindano na dawa pia vimevuruga taratibu za maabara na upasuaji mdogo mdogo. Endelea kuangalia na kusikiliza... Habari inatokana na vyanzo mbalimbali vya habari #sudan #raia #omdurman #afya #huduma #uhabawamadawa #matibabu #voa #voaswahili - - - - - #VOASwahili Sauti ya Amerika - Idhaa ya Kiswahili inawafikia zaidi ya watu milioni 100 wanaotembelea tovuti, mitandao ya kijamii, radio na televisheni zetu. Tunawasilisha maudhui kuhusu Afrika Mashariki na Kati kwa nchi takriban 11 huko Afrika na wale walioko ughaibuni na kwingineko duniani. Vipindi vyetu vimejikita katika maudhui mbalimbali ikiwemo habari, vijana, wanawake, siasa, sayansi, teknolojia, afya, biashara, michezo, muziki na burudani na pia tunawashirikisha wasikilizaji wetu.