Raila ashtumu rais Ruto kwa kushindwa kuwatengenezea ajira wakenya

  • | K24 Video
    159 views

    Wakati huohuo kinara wa Azimio Raila Odinga amemshtumu rais William Ruto kwa kushindwa kuwatengenezea ajira wakenya na kuwaacha kung'ang'ania ajira ughaibuni. Odinga pia amemkashifu Rais Ruto kwa kuendelea kushusha hadhi ya nchi kupitia juhudi zake za hadharani za kuwatafutia wakenya ajira katika mataifa ya kigeni anayozuru mara kwa mara. Kiongozi huyo wa upinzani amesema hayo wakati akiwahutubia wanafunzi wa chuo kikuu cha katoliki jijini Nairobi katika harakati za kusherehekea miaka 60 ya kenya kujitawala