Raila asisitiza NG-CDF kusimamishwa na Magavana

  • | Citizen TV
    2,222 views

    Kinara wa ODM Raila Odinga ameendeleza msukumo wake kuwa hazina ya ustawishaji maendelea ya maeneo bunge nchini CDF inapaswa kusimamiwa na magavana. Akizungumza katika kongamano la mahasibu mjini Mombasa, Odinga ametetea pendekezo lake akisema hatua za kuhalalisha hazina hiyo ni sharti ipitie kwa njia ya kura ya maamuzi. Mwenyekiti wa kamati ya bajeti bungeni Kimani Kuria hata hivyo amemkosoa Odinga akisema magavana na serikali za kaunti tayari wanakumbwa na usimamizi mbaya wa fedha za umma.