Rais aagiza waajiri kutekeleza nyongeza ya 6% ya mishahara

  • | Citizen TV
    1,990 views

    Rais William Ruto amewaagiza waajiri ambao hawajatekeleza nyongeza ya asilimia sita ya mishahara iliyotangazwa mwaka uliopita kufanya hivyo mara moja. Kwenye maadhimisho ya siku ya leba dei katika bustani ya Uhuru Gardens jijini Nairobi, Rais Ruto amesema haikubaliki kwa waajiri kutotekeleza nyongeza hiyo. Wawakilishi wa waajiri - fke- hawakupewa nafasi ya kuzungumza na wafanyikazi kwenye maadhimisho hayo ambapo rais ruto alitumia fursa hiyo kuratibu mafanikio ya serikali na kunadi mswada wa fedha wa mwaka wa 2025.