- 2,020 viewsDuration: 1:50Rais William Ruto amepuzulia mbali shutuma kutoka kwa umoja wa Upinzani kuhusu uongozi wake kwa kusema kwamba utendakazi wake uko imara. Akizungumza kwenye hafla ya kufunga mashindano ya Gofu ya Kenya Open, jijini Nairobi, rais Ruto alisema uongozi wake unaendelea kutoa huduma katika sekta muhimu zikiwemo Elimu, Uchumi, Afya, Usalama na Uchukuzi. Rais akisema miradi mbali mbali inayotekelezwa kama vile ujenzi wa barabara, masoko, reli na viwanja, inalenga kuinua miundombinu ya taifa, na kuelekeza uchumi wa taifa kufikia viwango vya mataifa yaliobobea kama vile Singapore.