- 572 viewsDuration: 2:22Rais William Ruto amezindua rasmi usambazaji wa shilingi milioni 220 za kuanza biashara ndogo chini ya hazina ya NYOTA kwa jumla ya vijana 8,000 kutoka kaunti za Kisumu, Siaya na Homabay. Akizungumza katika uwanja wa Jomo kenyatta mjini Kisumu, Rais Ruto amesema kwamba hatua hiyo ni mojawapo ya mikakati serikali imeweka kuangazia maswala yanayokumba vijana nchini kama vile ukosefu wa ajira. Vijana hao 8,000 wanajumuishwa kutoka jumla ya wadi 105 katika kaunti za Kisumu, Siaya na Homabay.