Rais aunga mkono wito wa kuunda serikali ya vyama vingi

  • | Citizen TV
    5,478 views

    Rais William Ruto amesema kwamba marekebisho ya uongozi wa serikali kuu hayawezi kuahirishwa huku akitangaza rasmi kwamba ataleta pamoja vyama vyote vya kisiasa kwa lengo la kuunda baraza la mawaziri ambalo litajumuisha Wakenya kutoka matabaka mbalimbali. Aidha, Naibu Rais Rigathi Gachagua amesema kwamba hatua ya kuvunjiliwa mbali kwa baraza la mawaziri inampa rais Ruto fursa ya kuteua mawaziri waliofuzu serikalini. Seth Olale ana tarifa kamili.