- 20,593 viewsDuration: 57sKiongozi mwenye umri wa miaka 92, Paul Biya wa Cameroon ametangazwa mshindi wa uchaguzi mkuu na kupanua uongozi wake ambao kwa sasa ni miaka 43. Kulingana na tangazo la tume ya uchaguzi nchini Cameroon, Biya ameshinda uchaguzi huo kwa jumla ya asilimia 54 ya kura zote zilizopigwa. Kiongozi wa upinzani Issa Tchiroma Bakary anasema watu wawili wameuawa na wavamizi mbele ya nyumba yake huko Garoua, huku mvutano ukizidi baada ya uchaguzi. Awali, Tchiroma alikuwa amejitangaza mshindi wa uchaguzi huo. Hali ya taharuki imeshuhudiwa katika miji mikubwa nchini humo huku baadhi wakijitokeza barabarani kupinga ushindi wa Biya. Kwa haya na mengine mengi ungana na @PMwangangi_ kwenye Dira ya Dunia TV mubashara saa tatu usiku kupitia ukurasa wa YouTube wa BBC Swahili. - - #bbcswahili #cameroon #uchaguzi2025 #siasa