- 14,221 viewsDuration: 3:28Rais William Ruto ameapa kukabiliana na matapeli wanaozuia mabadiliko katika Jiji la Nairobi akiwaarai wawakilishi wodi wa Nairobi kusimama naye na kusaidia kufanikisha mkataba wa makubaliano na serikali ya kitaifa. Akiwahutubia wawakilishi hao leo katika Bunge la Kaunti ya Nairobi, Rais Ruto alifunguka kuhusu namna ambavyo sehemu ya ukuta wa Ikulu ya Nairobi imejengwa kwenye mkondo wa maji akiahidi kubomoa ukuta huo katika harakati za kuzuia mafuriko Nairobi.