Rais William Ruto ameahidi kuongoza miradi ya maendeleo ili kufanikisha ukuaji wa kiuchumi na kijamii katika eneo la Ukambani. Akizungumza wakati wa sherehe ya siku kuu ya mashujaa katika uwanja wa michezo wa Ithookwe kaunti ya Kitui, Ruto aliahidi kutembelea eneo hilo kwa ziara ya kikazi katika muda wa majuma mawili yajayo. Wakati uo huo, aliwakosoa wale aliodai wanaeneza siasa za migawanyiko katika eneo hilo, hatua iliyosema imeathiri maendeleo kwa muda mrefu. Alitoa wito kwa eneo hilo kuendelea kuwa na umoja na kujitenga na viongozi wakabila.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive