Rais Ruto akutana na maseneta na wabunge wa Kenya Kwanza

  • | K24 Video
    115 views

    Rais William Ruto amekutana na wabunge na maseneta wa muungano wake wa kenya kwanza tayari kuanza kutekeleza mapendekezo ya kinara wa Azimio Raila Odinga kuhusu kuunda upya tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC. Kiongozi wa wengi bungeni Kimani Ichungwah anaongoza wabunge wa bunge la taifa wa kenya kwanza naye Aaron Cheruiyo akiongoza wale wa seneti . Kinara wa Azimio Raila Odinga pia anatarajiwa kufanya kikao kama hicho kutoa mwelekeo kwa wabunge wa Azimio. Hata hivyo, wataalamu wa kisheria wanasema wabunge watalazimika kubadilisha sheria kuhusu uteuzi wa jopo la uteuzi makamishena kabla ya kuendelea na mchakato