Rais Ruto apuuza habari kuwa hustler fund haina manufaa

  • | Citizen TV
    103 views

    Rais william Ruto leo amekutana na wawekezaji katika sekta ya kibinafsi kujadili mbinu mwafaka za kufanya biashara katika sekta hiyo. Mkutano huo umefanyika wakati ambapo serikali ikijifua kuwa uchumi umeimarika lakini wakati huo huo wafanyibiashara wakilalama kuwa mazingira ya kufanya biashara nchini ni magumu. Rais Ruto ametumia fursa hiyo kutetea hustler fund akisema imefaidi wakenya wengi licha ya habari kuwa serikali imepoteza zaidi ya shilingi bilioni 10 kutokana na watu kutolipa mikopo hiyo