Rais Ruto na naibu wake Gachagua wasema maandamano yanafadhaliwa

  • | K24 Video
    92 views

    Rais William Ruto na naibu wake Rigathi Gachagua wameilaumu iliyokuwa serikali ya handisheki kwa ghasia zinazokumba nchi. Kulingana nao uharibifu uliofanyika jana wakati wa maandamano ulikuwa umepangwa na kufadhiliwa kwa lengo la kulemaza utendakazi wa serikali ya kenya kwanza. Rais Ruto amesema kuwa serikali yake haitaruhusu uharibifu ulioshuhudiwa kuendelea na kamwe hatakubali handisheki na Odinga.