Rais William Ruto amewahimiza Wakenya wasio na vitambulisho watumie nafasi iliyotolewa na serikali ya kufutilia mbali ada za maombi ya kupata hati hiyo muhimu. Rais, aliyezungumza katika kaunti ya Vihiga wakati wa ziara yake ya maendeleo katika eneo la Magharibi, alisema hatua hiyo itawawezesha wananchi kupata huduma za serikali kwa urahisi na kunufaika na mipango ya kitaifa. Vilvile, aliwahimiza Wakenya wasajiliwe katika halmashauri ya afya ya kijamii ili kuhakikisha kila mtu anapata huduma za afya bila vikwazo.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive