Rais Uhuru Kenyatta azindua mashindano ya Safari Rally

  • | Citizen TV
    7,281 views

    Mashindano ya kimataifa ya mbio za magari ya Safari Rally yaling'oa nanga rasmi baada ya rais Uhuru Kenyatta kuhudhuria hafla hiyo leo mchana katika ukumbi wa KICC. Huu ni mwaka wa pili ambapo Kenya inaandaa mashindano hayo baada ya kujumuishwa katika msururu wa kimataifa mwaka jana na shirikisho la dunia la mbio za magari. Madereva zaidi ya thelathini wa kimataifa wako nchini kushiriki mashindano hayo ambayo yanaanza leo na kukamilika Jumapili ijayo katika eneo la Naivasha. Madereva hao watashiriki kitengo cha kwanza katika eneo la uwanja wa Kasarani kuanzia saa nane mchana. Dereva kutoka Finland Kalle Rovanpera ndiye anayeongoza jedwali baada ya kutwaa ushindi katika mashindano ya Sweden, Croatia na Ureno.