- 643 viewsDuration: 3:20Zaidi ya asilimia 98 ya wakenya waliotoa mlungula mwaka wa 2025 hawakuripoti visa hivyo. Hayo ni kulingana na ripoti mpya ya ufisadi iliyotolewa na Tume ya Kupambana na Ufisadi Nchini EACC ambayo imedhihirisha kuwa asilimia 73 ya wakenya hawana imani na jinsi serikali inapambana na ufisadi. Ripoti hiyo aidha imedokeza kuwa wanawake wako kwenye hatari zaidi ya kutoa rushwa na kunyanyaswa kingono licha ya kuwa wengi wao hawaripoti visa hivyo.