Ripoti ya ukaguzi wa wafanyikazi kaunti ya Elgeyo Marakwet yabaini kuwa ina wafanyikazi 112 hewa

  • | Citizen TV
    299 views

    Gavana Wa Kaunti ya Elgeyo Marakwet Wisley Rotich amepokea ripoti ya ukaguzi wa wafanyikazi ambayo imebaini kuwa kaunti hiyo ina wafanyikazi hewa 112 .Aidha Ripoti hiyo ilionyesha udhaifu kwenye usimamizi wa rasilimali na wafanyikazi wa Serikali ya Kaunti hiyo. wafanyakazi 112 waliotajwa kuwa hewa hawakuhudhuria zoezi la ukaguzi. Gavana Rotich alitangaza kuundwa kwa Kamati ya Utekelezaji ili kushughulikia masuala yote yaliyotajwa kwenye ripoti hiyo.