- 15,140 viewsDuration: 2:48Takriban asilimia 70 ya miradi ya ujenzi wa nyumba za bei nafuu imejengwa kwenye ardhi isiyo na hati miliki, ikiweka hatarini miradi hiyo ikiwa haitapata stakabadhi hizo muhimu kwa wakati unaofaa. Hayo ni kwa mujibu wa ripoti maalum ya hivi punde ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Dkt. Nancy Gathungu, aliyeiambia Kamati ya Uhasibu ya Bunge la Kitaifa kwamba miradi hii iko kwenye hatari ya kukabiliwa na changamoto za kisheria katika siku za usoni.