- 3,976 viewsDuration: 2:42Rais William Ruto amesema kuwa hahitaji ruhusa ya yeyote kuzuru eneo la mlima kenya na kutafuta uungwaji mkono na wakazi wa eneo hilo. Akizungumza wakati wa ziara yake huko Murang'a, Rais Ruto amewasuta viongozi anaosema wamejitwika mamlaka ya kuwa madalali wa kura za wakazi akisema wanamlima watajiamulia wenyewe watakayempigia kura ya urais. Viongozi wa mlima Kenya walioandamana na Rais walimnadi naibu wake Profesa Kithire Kindiki kama mgombea mwenza wa Rais Ruto kwenye uchaguzi ujao.