- 3,915 viewsDuration: 3:22Rais William Ruto anasisitiza ukaribu wake na eneo la Mlima Kenya licha ya baadhi ya wapinzani wake kudai kuwa amesaliti na kupuuza maendeleo aliyoahidi kufanya katika eneo hilo. Kwenye mkutano na viongozi pamoja na baadhi ya wakazi wa Kaunti ya Kirinyaga, Rais Ruto amesema kuwa licha ya kuunda serikali jumuishi na viongozi wa chama cha ODM, hajasahau ahadi zake kwa eneo la Mlima Kenya. Rais Ruto amesema hawezi kamwe kuitenga Mlima Kenya na kuwataka wakazi wa eneo hilo kumpa fursa ya kutenda zaidi kwenye muhula wake wa pili.