Shirika la Samaritan's Purse limethibitishia kuwa wafanyakazi wake saba raia wa Marekani waliokuwa wakishiriki kudhibiti mlipuko wa Ebola nchini DRC wamekuwa nchini Kenya kwa siku tano zilizopita. Wafanyakazi hao wanatekeleza karantini ya lazima ya siku 21 katika kituo cha karantini ya Ebola kilichopo katika kambi ya jeshi ya Laikipia mjini Nanyuki. Afisa Mkuu wa shirika hilo la kanisa, Franklin Graham, amesema alizungumza na saba hao siku mbili zilizopita wakiwa Laikipia. Na kama anavyoarifu Emily Chebet, Serikali ya Kenya haijatoa taarifa yoyote kuhusiana na suala hilo.