Seneti kujadili hoja ya kumuondoa Gachagua jumatano

  • | Citizen TV
    1,177 views

    Akina mama katika kaunti ya Busia wamewataka wakenya kwa jumla kuwa na subira kufuatia hoja inayoendelea ya kumbandua naibu rais Rigathi Gachagwa mamlakani, wakisema kuwa ni swala linaloendelea kuwakanganya wakenya.Wakizungumza mjini Busia, kina mama hao wamesema kuwa wana imani kuwa sheria itafuatwa ipasavyo na nchi kurejelea hali yake ya kawaida. seneti itaanza kusikiza hoja hiyo siku ya jumatano wiki hii.