Mwongozo wa Afya ya Akili kwa viongozi wa kidini umezinduliwa jijini Mombasa, ukiwa na lengo la kuimarisha mchango wa taasisi za kidini katika kutambua na kushughulikia changamoto za afya ya akili.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mwenyekiti wa Hospitali ya Chiromo, Profesa Frank Njenga, amesema kwa muda mrefu imani tiba zimekinzana, hali ambayo imesababisha wengi kuendelea kuhangaika na matatizo ya afya ya akili bila kupata msaada unaofaa. Wakati uo huo, Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana nchini, Dkt. Jackson Ole Sapit, amekashifu shambulizi lililotokea katika Kanisa la St Peter’s ACK Witima mjini Othaya, akilitaja kama kitendo kinacho kandamiza demokrasia nchini.