Serikali haitaingilia mzozo wa ardhi ya Kirima

  • | Citizen TV
    3,180 views

    Serikali haitaingilia mzozo wa ardhi kati ya familia ya mwanasiasa wa zamani marehemu Gerishon Kirima. Waziri wa Ardhi Alice Wahome amesema uamuzi wa mahakama utaheshimiwa na kuwa rekodi za wizara ya ardhi zimethibitisha kwamba shamba hilo ni la familia ya marehemu Kirima. Na kama anavyoarifu Mary Muoki, Waziri huyo amewataka maskwota hao wafanye mazungumzo na familia ya Kirima au waondoke.