Skip to main content
Skip to main content

Serikali imezindua ofisi zaidi za utawala eneo la Tarbaj

  • | Citizen TV
    247 views
    Duration: 1:04
    Serikali imezindua ofisi zaidi za utawala katika Eneo bunge la Tarbaj, hatua inayolenga kusongeza huduma za serikali karibu na wananchi pamoja na kuimarisha usalama. Kata za Dashek na Haragal sasa zimeanzishwa rasmi, zikitarajiwa kushughulikia changamoto za kipekee za kiutawala na kiusalama katika eneo hilo. Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mbunge wa Tarbaj, Hussein Abdi Barre, alimshukuru Rais William Ruto na serikali ya kitaifa kwa hatua hiyo, huku akiwahimiza wananchi kuendelea kuunga mkono serikali inayowahudumia kwa ufanisi.