Serikali kupitia Idara ya utamaduni sasa inapanga kukarabati madhabahu ya Mukurwe wa Nyagathanga yaliyoko Kaunti ya Murang’a, eneo linaloaminika kuwa chimbuko la jamii ya Agikuyu.
Mukurwe wa Nyagathanga ni pahali ambapo pamehifadhiwa na kuthaminiwa na jamii. Serikali kupitia Idara ya Utamaduni na Urithi imeweka mikakati ya kukarabati na kuboresha madhabahu hayo. Akizungumza wakati wa tamasha la vipaji na utamaduni lililoandaliwa Kiharu, Katibu katika wizara ya michezo, Elijah Mwangi, anasema ukarabati huo unalenga kuhifadhi urithi wa kitamaduni na kuimarisha maeneo ya kihistoria ambayo yana umuhimu mkubwa kwa jamii.