- 3,456 viewsDuration: 3:02Serikali sasa inasema sio kila mtu anayetaka kupewa dawa mpya za kuzuia maambukizi ya virusi vya HIV, atapewa dawa hizo. Badala yake, kuna masharti ambayo ni lazima yatimizwe kwanza kabla ya mtu kupewa dawa hiyo. Haya yamebainika kwenye kikao cha afya hapa Nairobi ambapo pia tahadhari imetolewa kwa wanaotumia dawa za kuongeza nguvu za kiume kwamba huenda wakapata changamoto za kiafya iwapo watatumia dozi ya juu ya dawa hii ya kuzuia HIV.