Serikali yaendelea kutetea makato ya nyumba za bei nafuu

  • | K24 Video
    4 views

    Hayo yakijiri, serikali imeendelea kutetea makato ya nyumba za bei nafuu. Kupitia katibu mkuu wa makazi Charles Hinga, serikali imesema makato hayo sio ushuru ila ni akiba itakayowezesha serikali kuwajengea wananchi nyumba za bei nafuu. Hata hivyo, hinga ameelezea kuwa hata baada ya kurejeshewa fedha hizo baada ya miaka saba, ada hiyo bado itaendelea kutozwa. Muajiriwa atarejeshewa asilimia 3 aliyokatwa katika mshahara kila mwezi ila mchango wa muajiri utarudishiwa mfanyikazi baada ya miaka 14. Rais William Ruto amewarai wabunge wa muungano wake wa Kenya Kwanza kupitisha mswada huo tarehe 15 mwezi ujao.