Sekta ya wafanyakazi inahimiza ongezeko la ufadhili ili kufanikisha mafunzo ya kikazi na uidhinishaji wa wataalamu wa sekta hiyo. Wakiongozwa na afisa mkuu mtendaji wa bodi ya mitihani ya kitaaluma ya maafisa wa idara za wafanyakazi Margaret Nguu, maafisa hao wanasema hata ingawa sekta hiyo hupokea ufadhili wa serikali, ipo haja ya kutengewa fedha zaidi ili taasisi zinazotoa mafunzo hayo ziweze kuwasajili wataalamu zaidi na kuhakikisha Wakenya zaidi wanapata ujuzi hitajika. Haya yaliibuliwa wakati bodi hiyo ilipotangaza matokeo ya mtihani wa kitaifa wa mafunzo ya wataalamu wa idara za wafanyakazi.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN
Follow us on Twitter: https://twitter.com/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1tv
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#KBCchannel1 #Kenya #News