Skip to main content
Skip to main content

Serikali yahimizwa kuongeza mgao wa fedha kwa walemavu

  • | Citizen TV
    104 views
    Serikali imetakiwa kuongeza mgao wa fedha za kuwasaidia wanaoishi na ulemavu nchini kutokana na changamoto kubwa zinazowakumba wazazi katika kuwapata watoto hao mahitaji muhimu. Wakizungumza katika eneo la Sikhendu, kaunti ya Trans Nzoia, wadau mbalimbali wamesema kuna haja ya serikali kuweka mikakati madhubuti kuhakikisha familia zenye watoto wanaoishi na ulemavu zinapata usaidizi ili kupunguza mzigo wa maisha na dhiki wanazopitia kila siku. Wadau hao pia wamewataka wazazi kuacha kuwaficha watoto wenye ulemavu na badala yake kuwapeleka shule pamoja na vituo vya afya ili wapate huduma mwafaka.