Serikali yaidhinisha fedha za kukarabati uwanja wa Nyayo kabla ya Kip Keino Classic

  • | K24 Video
    35 views

    Ni afueni kwa wanariadha nchini Kenya baada ya mwenyekiti wa maendeleo ya vijana wa riadha Kenya, Barnaba Korir, kuthibitisha kuwa serikali imeidhinisha fedha kwa ajili ya usakinishaji wa uso mpya wa uwanja kabla ya mashindano yanayosubiriwa kwa hamu ya Kip- Keino Classic Continental tour yatakayofanyika mei 31. Korir alikuwa akizungumza katika uwanja wa kitaifa wa nyayo wakati wa ugawaji wa nambari za usajili kwa wanariadha waliyoalikwa kushiriki katika majaribio ya kuwania nafasi ya kushiriki mashindano ya World Relay Championship yatakayofanyika kesho katika uwanja huo huo wa Nyayo.