- 110 viewsWizara ya Kawi imetupilia mbali ombi la Kampuni ya Umeme ya Kenya Power kupandisha bei ya umeme nchini kuanzia mwezi Julai mwaka huu. Kenya Power ilikuwa imewasilisha ombi la kuongeza bei ya umeme kwa mamlaka ya kudhibiti gharama ya kawi, EPRA, na shughuli ya kukusanya maoni ya wananchi ilitarajiwa kuanza. Waziri wa Kawi Opiyo Wandayi amesema bei iliyopo sasa itaendelea kutumika ili kuwakinga Wakenya.