Serikali yapiga marufuku matangazo mubashara kuhusu maandamano

  • | BBC Swahili
    2,018 views
    Maadhimisho ya mwaka mmoja tangu vijana kuawa bungeni walipovamia majengu ya bunge yameshuhudia ghasia kubwa katika miji mbali mbali nchini Kenya, hasa Nairobi. Vijana waliojitokeza kwa wingi wanaitaka serikali kuwasikiliza hasa kuhusiana na suala la wao kutekwa nyara na kuawa katika hali tatanishi mikononi mwa polisi. @RoncliffeOdit anaangazia maandamano haya ambayo yameilazimu serikali kupiga marufuku matangazo ya moja kwa moja ya runinga kuhusu maandamano hayo. Jiunge naye mubashara kwenye Dira ya Dunia TV kwenye ukurasa wa YouTube BBC Swahili #bbcswahili #kenya #diratv Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw