Serikali yatakiwa itilie mkazo mafunzo ya stadi za maisha

  • | K24 Video
    20 views

    Chama cha kitaifa cha wazazi kwa ushirikiano na wadau mbalimbali katika sekta ya elimu wameelezea haja ya mafunzo kuhusu stadi za maisha kujumuishwa kama somo katika mtaala mpya wa elimu. Wadau hao wamehusisha ukosefu wa maadili mema miongoni mwa kizazi cha sasa kwa sera ambazo haziorodheshi somo hilo shuleni. Wizara ya elimu sasa imeshinikizwa kufanya marekebisho na kutoa vifaa tosha vya kufunza somo hilo.