Skip to main content
Skip to main content

Serikali yatangaza kafyu Transmara kufuatia mauaji na taharuki Angata Barrikoi

  • | Citizen TV
    2,917 views
    Duration: 3:11
    Naibu inspekta jenerali Eliud Langat ametamgaza amri ya kutotoka nje maeneo kumi na matano Transmara Kusini na Magharibi kutokana na machafuko yanayoendelea kushuhudiwa Angata Barrikoi. Katika kikao maalum na maafisa wa usalama, Lagat ameongeza kuwa watu wanaomiliki bunduki haramu wana muda wa chini ya saa 72 kuzisalimisha. Na kama anavyoripoti mwanahabari wetu Chrispine Otieno mtu mmoja aliuawa usiku wa kuamkia leo eneo la Angata baada ya kupigwa risasi na wahuni.