- 794 viewsDuration: 2:05Ahadi za afya bora kwa wote chini ya bima ya SHA zimegeuka msumari wa moto kwenye vidonda vya wagonjwa wanaotafuta matibabu ya kitaalamu ughaibuni. Ndio hali inayomkabili mwalimu mmoja ambaye amejipata kwenye njia panda katika hospitali moja nchini India ambako amekuwa akisubiri matibabu kwa miezi mitatu.