SHA Yakosa Mapato, Mercy Mwangangi Kuiongoza

  • | K24 Video
    397 views

    Mamlaka ya Afya ya Jamii (SHA) inakabiliwa na upungufu mkubwa wa mapato, kwani ni Wakenya milioni 4 pekee kati ya milioni 22 waliojisajili ndio wanaochangia kifedha. Wadau wanasema hofu kuhusu mfumo mpya wa SHA imeathiri usajili na imani ya umma. Wakati huo huo, Mercy Mwangangi ameteuliwa kuwa Afisa Mkuu Mtendaji wa SHA, akipewa jukumu la kuimarisha mfumo huo na kutekeleza mpango wa bima ya afya kwa wote.