Shirika la Kutunza Mazingira latia saini mkataba na wafugaji katika kaunti ya Kajiado

  • | Citizen TV
    357 views

    Shirika moja la kutunza mazingira limetia saini mkataba na kundi la malisho la Olgulului katika kaunti ya Kajiado wa kuhakikisha kuwa wanachama wa kundi hilo la malisho wanatunza nyasi na mimea mingine kwenye ardhi yao ili kupunguza usalishaji wa hewa ya kaboni kwenye mazingira katika eneo hilo. Kundi hilo litapokea shilingi Millioni 37M kila mwaka na kutakiwa kuhakikisha linawalisha mifugo kwa njia ambayo mimea haitaisha kabisa kwenye ardhi pia wakitakiwa kutokata miti.