Shughuli za biashara zatatizika mtaani Eastleigh baada ya kizaazaa cha maziwa

  • | Citizen TV
    5,013 views

    Shughuli za biashara katika mtaa wa Eastleigh hapa jijini Nairobi zilitatizika mchana kutwa baada ya wafanyibiashara kukabiliana na maafisa wa usalama waliokuwa wakiendesha oparesheni ya kunasa maziwa ya poda. Wafanyibiashara waliojawa na ghadhabu walidai kulengwa na maafisa wa usalama kufuatia oparesheni ambazo zimekuwa zikiendelea tangu mwaka jana.