Skip to main content
Skip to main content

Shule za Westlands zanufaika na mradi wa maji

  • | KBC Video
    46 views
    Duration: 2:49
    Mbunge wa Westlands Timothy Wanyonyi amekabidhi visima viwili kwa shule ya sekondari ya North Highridge Comprehensive na ile ya Westlands Comprehensive katika wadi za Parklands na Highridge mtawalia. Mpango huo unanuiwa kukabiliana na uhaba wa maji uliokumba shule hizo ambao ulisababisha kuvurugwa kwa shughuli za masomo na kuzidisha mzigo kwa rasilmali za shule. Akizungumza wakati wa hafla ya kuvikabidhi mbunge huyo alisema kuwa visima hivyo vilivyo na mabomba, mifumo ya kielektroniki ya utumiaji na mitambo ya kawi ya jua vilichimbwa na kwekwa vifaa hivyo wakati wa msimu wa sikukuu ya krismasi na hivyo kuepusha kuvurugwa kwa shughuli za masomo. Wanyonyi aliongeza kusema kuwa visima hivyo vitatoa suluhu ya kudumu kwa shule hizo na pia kwa jamii ya eneo hilo. Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/ #kbcchannel1 #news #kbclive