Shule zakabidhiwa vifaa vya kutambua matatizo ya afya

  • | Citizen TV
    290 views

    Walimu kutoka shule za umma wamepatiwa mafunzo maalum kuhusu masuala ya afya ya msingi shuleni, ikiwa ni pamoja na utambuzi wa dalili za utapia mlo, kupima shinikizo la damu na matumizi ya dawa za huduma ya kwanza kwa wagonjwa wa dharura. Mafunzo hayo yameendeshwa kama sehemu ya mpango wa kuboresha huduma za afya ya msingi kwa wanafunzi shuleni, hasa maeneo ya mashinani ambayo mara nyingi hukumbwa na changamoto za kiafya. Kupitia mpango huo, walimu walifundishwa jinsi ya kutambua ishara za lishe duni, kupima na kufuatilia afya ya wanafunzi, na kutoa msaada wa haraka kabla ya wagonjwa kufikishwa katika vituo vya afya.