Skip to main content
Skip to main content

'sichangamani na wanasiasa naogopa'

  • | BBC Swahili
    5,557 views
    Duration: 2:44
    Wakati Tanzania ikitarajiwa kufanya uchaguzi mkuu siku ya Jumatano, hofu bado ipo kwa baadhi ya watu wenye ualbino kama Mariam Staford ambaye aliwahi kufanyiwa ukatili kwa kukatwa mikono yake mwaka 2008. Tukio la kukatwa kwake mikono, kama yalivyo matukio mengine ya aina hiyo yanahusishwa na imani za potofu kwamba viungo vya watu wenye ualbino vinaweza kuleta utajiri au mamlaka za kisiasa. Hali hiyo imechangia katika mauaji, kujeruhi na pia wakati mwingine ufukuaji wa makaburi walipozikwa watu hao. Kwa mujibu wa Taasisi ya kutetea haki za binadamu ya ‘Under the Same Sun’, zaidi ya visa 200 vya watu wenye ualbino kushambuliwa vimerekodiwa katika kipindi cha miaka 16 iliyopita nchini Tanzania, huku baadhi ya familia zikilazimika kukimbia au kuishi mafichoni. Serikali inasema inachukua hatua kukabili hali hiyo. Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw