Siku ya maji ulimwenguni kuadhimishwa Turkana

  • | Citizen TV
    220 views

    Ulimwengu unapojiandaa kwa siku ya maji ijumaa wiki hii,maadhimisho ya kitaifa yamepangiwa kufanyika katika mji wa Kakuma kaunti ya Turkana. Kaunti hiyo ni mojawapo ya maeneo kame nchini ambayo yameshuhudia migogoro ya kijamii yanayochochewa na uhaba wa maji. kauli mbiu ya mwaka huu ikiwa ni umuhimu wa maji kwa kukuza amani, kaunti ya turkana imeanza kuwekeza kwenye miradi ya kuvuna na kusambaza maji ili kuzuia vita vya mara kw amara baina ya wafugaji.