Skip to main content
Skip to main content

Simulizi za kusikitisha za manusura wa mwisho katika Vita ya Biafra Nigeria

  • | BBC Swahili
    3,207 views
    Duration: 26:36
    Baadhi ya manusura wa mwisho wa Vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Nigeria, vinavyojulikana pia kama Vita vya Biafra, wanashiriki kumbukumbu zao za walichoshuhudia wakiwa mstari wa mbele wa mapigano. Jiunge na chaneli yetu hapa 👉🏽https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw Wengi wa manusura wa Vita vya Biafra sasa wana umri wa miaka ya 70 na 80. Maumivu na athari za vita hivyo vimewafanya wengi wao kushindwa kusimulia hadithi zao kwa miongo kadhaa. Huku muda ukiendelea kuyoyoma, kuna umuhimu wa kuhifadhi kumbukumbu zao kabla hazijapotea. Filamu hii ya makala imeongozwa na watengenezaji filamu wa Nigeria walioshinda tuzo, Meji na Leke Alabi, ambao babu yao, aliyekuwa Kamando mwandamizi wa Jeshi la Shirikisho la Nigeria, alishiriki katika vita hivyo. Inakadiriwa kuwa kati ya watu 600,000 hadi milioni 3 walifariki nchini Biafra, huku kukiwa na tuhuma za kutendeka kwa uhalifu wa kivita. Kupitia simulizi zenye hisia kali kutoka kwa mashuhuda wa mstari wa mbele, zikichanganywa na kumbukumbu kubwa za video za BBC ambazo nyingi hazijawahi kuonekana hadharani, makala hii inaangazia vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoathiri maisha ya mamilioni ya watu na ambavyo vinaendelea kuathiri mijadala nchini Nigeria hadi leo. Makala hii imetayarishwa na BBC Africa Eye kwa ushirikiano wa wataalamu kutoka BBC Igbo Service, na inajumuisha simulizi za mashuhuda kutoka pande zote mbili za mgogoro huo ili kutoa taswira pana ya historia hiyo. Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw